• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 23, 2016

  'MIKADI' YAMPONZA HIMID MAO 'NINJA' WA AZAM KUWAKOSA PRISONS KESHO SOKOINE

  Na David Nyembe, MBEYA
  AZAM FC itamkosa kiungo wake mahiri wa ulinzi, Himid Mao Mkami 'Ninja' katika wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine, kwa sababu atakuwa anatumia adhabu ya kadi tatu za njano.
  Lakini hakuna shaka, kiungo raia wa Ivory Coast, Kipre Michael Balou ataziba pengo hilo vizuri kesho Uwanja wa Sokoine.
  Nahodha huyo Msaidizi wa Azam FC alionyeshwa kadi ya tatu ya njano Jumamosi mjini Mbeya, wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City.
  Himid Mao 'Ninja' ataikosa mechi dhidi ya Prisons kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya

  Himid ambaye atarudi uwanjani kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Panone Jumapili Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, atakuwa huru kucheza pia kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga Machi 5.
  Wachezaji wengine wa Azam FC watakaoendelea kuikosa mechi hiyo ni mabeki Aggrey Morris, Abdallah Kheri na Racine Diouf  pamoja na mshambuliaji Didier Kavumbagu, waliokuwa majeruhi wakiendelea na maandalizi ya mwisho kurejea uwanjani.
  Azam FC inahitaji ushindi katika mchezo wa kesho ili kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, kwani itafikisha pointi 48 na kuwapiku mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 46. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'MIKADI' YAMPONZA HIMID MAO 'NINJA' WA AZAM KUWAKOSA PRISONS KESHO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top