• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 27, 2016

  SUNDAY OLISEH ABWAGA MANYANGA NIGERIA KISA 'KAZI BILA MUSHAHARA'

  KAMPENI za Nigeria kufuzu Fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zimeingiwa na majaribu tena, baada ya kocha Sunday Oliseh kujiuzulu jana kutokana na kutolipwa mishahara na kukiukwa kwa Mkataba wake.
  Oliseh, ambaye amefnya kazi kwa miezi minane tu katika Mkataba wake wa miaka mitatu, amesema amejiuzulu kutokana na kutopewa ushirikiano na Shirikisho la Soka Nigeria (NFF).
  "Kutokana na kutoheshimiwa kwa Mkatavba, kutopewa ushirikiano, kutolipowa mishahara, maslahi ya wachezaji wangu, makocha wasaidizi na mimi,najiuzulu ukocha Mkuuu wa Super Eagles,"amesema. 

  Sunday Oliseh amejiuzulu ukocha wa Super Eagles kutokana na kutolipwa mishahara na kukiukwa kwa Mkataba wake

  Oliseh, Nahodha wa zamani wa Super Eagles ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter mapema Ijumaa.
  Kocha aliyemuachia nafasi Oliseh, baada ya kuondoka Julai mwaka 2015, Stephen Keshi naye awali alilalamika kutolipwa mishahara kabla ya baadaye kulipwa na Rais wa Nigeria mwaka 2013.
  Wachezaji pia wamekuwa wakilalamikia kutolipwa posho zao na Oliseh anajiuzulu kiasi cha mwezi mmoja kabla ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri Kaskazini mwa Jiji la Kaduna na marudiano siku mbili baadaye mjini Cairo.
  Misri, mabingwa mara saba wa AFCON, lakini Oliseh amesema hakusafiri kwenda Ulaya ili kuwaangalia wachezaji wa Nigeria wa kuongeza kwenye kikosi chake.
  Katibu Mkuu wa NFF, Mohammed Sanusi, yupo Zurich, Uswisi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) uliofanyka jana, amethibitisha shirikisho kupokea barua ya kujiuzulu kwa Oliseh.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUNDAY OLISEH ABWAGA MANYANGA NIGERIA KISA 'KAZI BILA MUSHAHARA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top