• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 21, 2016

  CHELSEA YAPEWA EVERTON ROBO FAINALI KOMBE LA FA, ARSENAL IKIFUZU KUKUTANA NA WATFORD

  ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND
  Reading Vs Crystal Palace
  Everton Vs Chelsea
  Arsenal/Hull City Vs Watford
  Shrewsbury Town/Man Utd Vs West Ham

  West Ham United itamenyana na mshindi kati ya Shrewsbury Town na Manchester United watakaocheza kesho

  CHELSEA itamenyana na Everton katika Robo Fainali ya Kombe la FA England Uwanja wa Goodison Park, kufuatia kuitoa Manchester City kwa kuifunga mabao 5-1 usiku wa leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Crystal Palace ya mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor itasafiri kuifuata Reading baada ya kuitoa Tottenham Hotspur leo kwa kuifunga 1-0 Uwanja wa White Hart Lane.
  Watford itasafiri kuifuata Arsenal au Hull City, wakati West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.
  Arsenal watarudiana na Hull City kusaka timu ya kwenda Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates jana, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United kesho Uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.
  Mechi za Robo Fainali za Kombe la FA zitachezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAPEWA EVERTON ROBO FAINALI KOMBE LA FA, ARSENAL IKIFUZU KUKUTANA NA WATFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top