• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 24, 2016

  MCLEISH AMRITHI MIDO ZAMALEK, AL AHLY NAO WATAKA KUBADILI KOCHA

  KOCHA wa zamani wa Scotland ma Rangers, Alex McLeish (pichani kulia) amefikia makubaliano ya kufundisha klabu ya Zamalek ya Misri.
  Taarifa ya Zamalek jana iliyoifikia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imesema kwamba McLeish, ambaye pia amezifundisha Birmingham City, Aston Villa na Nottingham Forest za England, anachukua nafasi ya Ahmed Hassan 'Mido' aliyefukuzwa.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Misri na klabu ya Tottenham ya England alifukuzwa Zamalek wiki mbili zilizopita baada ya kufungwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa Jiji la Cairo, Al Ahly katika mchezo wa Ligi Kuu.
  "Tumefikia makubaliano na kocha Mscotland Alex McLeish kuiongoza timu ya kwanza,"amesema Rais wa Zamalek, Mortada Mansour.
  Mansour amesema kwamba McLeish atawasili Misri mara moja kusaini Mkataba na kuanza kazi.
  Vinara wa Ligi ya Misri, Al Ahly wanaweza pia kubadili kocha wakati wowote, baada ya magazeti nchini humo kuripoti kwamba wapo kwenye mazungumzo na Martin Jol.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MCLEISH AMRITHI MIDO ZAMALEK, AL AHLY NAO WATAKA KUBADILI KOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top