• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 20, 2016

  PLUIJM AWAPANGIA SIMBA MABEKI WATATU KATIKATI, NI BOSSOU, TWITE NA NGONYANI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ameanzisha mabeki watatu wa kati kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Pluijm amewaanzisha kwa pamoja kucheza katikati Mtogo Vincent Bossou, Mkongo Mbuyu Twite na mzalendo Pato Ngonyani.
  Langoni yupo Ally Mustafa ‘Barthez’, beki wa kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, wakati viungo ni Thabani Kamusoko, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima na washambuliaji ni Donald Ngoma na Amissi Tambwe.  
  Kikosi cha Yanga SC kilichoanza Septemba 26, mwaka jana Simba akifa 2-0

  Kikosi cha Yanga SC kinachoanza leo; Ally Mustafa ‘Barthez’ Juma Abdul, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
  Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Mwashiuya, Simon Msuva, Malimi Busungu na Issoufou Boubacar. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PLUIJM AWAPANGIA SIMBA MABEKI WATATU KATIKATI, NI BOSSOU, TWITE NA NGONYANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top