• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 22, 2016

  MAREFA WA ERITREA KUCHEZESHA YANGA NA CERCLE JUMAMOSI TAIFA

  MAREFA wa Eritrea ndiyo watachezesha mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Yanga SC na Cercle de Joachim ya Mauritius Jumamosi wiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba marefa watawasili nchini Jumatano.

  Amewataja marefa hao kuwa ni Amanuel Eyob Russo atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na Suleiman Ali Salih na Hugush Abdelkader Berhan Mohammed watakaoshika vibendera, wakati refa wa akiba mezani atakuwa Idrisa Mohammed Osman na Kamisaa Wiiliam Makinat wa Swaziland.
  Yanga SC ilishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza nchini Mauritius na Jumamosi watahitaji hata sare kusonga mbele.
  katika hatua nyingine, Muro amesema Yanga SC itaanza mazoezi leo jioni kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA Jumatano dhidi ya JKT Kanembwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA ERITREA KUCHEZESHA YANGA NA CERCLE JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top