• HABARI MPYA

    Wednesday, February 17, 2016

    CAVANI AIFUNGIA LA USHINDI PSG IKIILAZA CHELSEA 2-1 PARIS LIGI YA MABINGWA

    Mshambuliaji Edinson Cavani (kulia) akishangilia na David Luiz baada ya kuifungia PSG bao la pili dakika ya 78 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea usiku huu Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Bao lingine la Paris Saint Germain limefungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39 baada ya shuti lake la mpira wa adhabu kumbabatiza kiungo Mnigeria, John Obi Mikel na kutinga nyavuni. Mikel alifuta makosa yake kwa kuifungia The Blues bao la kusawazisha dakika ya 45 na timu hizo zitarudiana Machi 9, Uwanja wa Stamford Bridge na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 
    PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mshambuliaji wa Benfica, Konstantinos Mitroglou (katikati) akifumua shuti kuifungia bao pekee timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Zenit St Petersburg katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAVANI AIFUNGIA LA USHINDI PSG IKIILAZA CHELSEA 2-1 PARIS LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top