Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
KIUNGO Said Juma ‘Makapu’ (pichani kulia) leo hakufanya mazoezi na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Uwanja wa Olimpia Park mjini hapa kutokana na maumivu ya mgongo.
Stars imefanya mazoezi kwa siku ya pili leo mjini Rustenburg, Afrika Kusini kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa COSAFA Jumatatu dhidi ya Swaziland.
Na kiungo huyo chipukizi anayeinukia vizuri aliumia akiichezea klabu yake, Yanga SC katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara wiki iliyopita.
Makapu amabye kwao Zanzibar huitwa Kizota, akifananishwa na beki, kiungo na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ (sasa marehemu), leo alifanya mazoezi mepesi peke yake chini ya uangalizi wa Dakatri.
“Nina maumivu ya mgongo niliyoyapata katika mechi yetu ya mwisho ya Ligi na Ndanda, na kwa hali hii ya baridi ya huku, sijui kama nitapata ahueni,”amesema.
Stars ipo Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Kombe la COSAFA, inayoanza Jumapili ikiwa imeweka kambi katika hoteli ya Hunters Rest, nje kidogo ya mji huu.
Mbali na Makapu, wachezaji wengine walio na Stars hapa ni makipa: Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Mwadini Ali (Azam), mabeki ni Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM).
Wengine ni viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam), Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar).
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba), Mrisho Ngassa (Free State Stars), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (ZESCO United).
Taifa Stars imepangwa pamoja na Lesotho, Swaziland na Madagascar na katika Kundi A, wakati Kundi B lina timu za Shelisheli, Namibia, Zimbabwe na Mauritius.
Kila timu itakayoongoza kundi, itaungana na wenyeji Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia kwa ajili ya hatua ya Robo Fainali.
Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia zimeingia moja kwa moja katika Robo Fainali kwa sababu zipo juu viwango vya ubora wa soka vya FIFA.

![]() |
| Kocha Mholanzi (katikati) akiwaongoza vijana wake mazoezini leo Uwanja wa Olimpia Park |
![]() |
| Wachezaji wa Stars wakifanya mazoezi mepesi leo Uwanja wa Olimpia Park |
Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia zimeingia moja kwa moja katika Robo Fainali kwa sababu zipo juu viwango vya ubora wa soka vya FIFA.

.png)
0 comments:
Post a Comment