Alvaro Morata hakutaka kushangilia baada ya kuifungia Juventus leo dhidi ya timu yake ya zamani, Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI kinda wa umri wa miaka 22 wa kimataifa wa Hispania, Alvaro Borja Morata Martin ameivua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya timu yake ya zamani, Real Madrid.
Morata ameifungia bao Juventus katika sare ya 1-1 na Real leo Uwanja wa Bernabeu katika Nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa. Juve sasa inasonga mbele kwa ushindi wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 mjini Turin.
Morata alitua kwa Kibibi Kizee cha Turin Julai 19 mwaka kwa dau la Euro Milioni 20 kwa Mkataba wa miaka mitano, huku Real Madrid ikipewa fursa ya kumnunua tena katika vipengele vya Mkataba.
Mechi ya kwanza alifunga pia dakika ya nane na mabao yake mawili yanakuwa mchango mkubwa kwa Juve kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambako watakutana na Barcelona iliyoitoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3.
Katika mchezo wa leo, Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo alianza kuifungia Real dakika ya 23 kwa penalti, baada ya Giorgio Chiellini kumuangusha James Rodriguez.
Alvaro Morata akaisawazishia Juve dakika ya 58 baada ya kukutana na mpira uliorudi kufuatia piga nikupigie iliyotokea langoni mwa Real, baada ya mpira wa adhabu.
Juventus mabingwa wa michuano hiyo mara mbili, 1985 na 1996, mara ya mwisho walifika fainali mwaka 2003 na kufungwa na AC Milan kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester.
Fainali ya mwaka huu ya Ligi ya Mabingwa itafanyika Uwanja wa Olympia mjini Berlin, Ujerumani Juni 6, 2015.
KIkosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Carvajal, Sergio Ramos, Varane, Marcelo, Rodriguez, Kroos, Isco, Bale, Benzema/Hernandez dk67 na Ronaldo.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Pogba/Pereyra dk89, Pirlo/Barzagli dk79, Marchisio, Vidal, Tevez, Morata/Llorente dk84.

.png)
0 comments:
Post a Comment