• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2015

    BAYERN MUNICH YAILAZA BARCA 3-2 ALLIANZ ARENA, LAKINI HAIJASAIDIA

    Lionel Messi (katikati) akienda chini katikati ya wachezaji wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger na Xabi Alonso katika mchezo wa leo

    BAYERN Munich imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Barcelona usiku huu Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya michuano ya mwaka huu.
    Matokeo hayo yanafanya Bayern iage kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-3, baada ya awali kufungwa 3-0 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
    Barca sasa itamsubiri mshindi wa jumla kati ya Juventus na Real Madrid ikutane katika fainali. Juve ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza.
    Mabao ya Bayern katika mchezo wa leo yamefungwa na Medhi Benatia dakika ya saba, 
    Robert Lewandowski dakika ya 59 na Thomas Muller dakika ya 74, wakati ya Barca yote yamefungwa na Neymar dakika ya 15 na 29.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAYERN MUNICH YAILAZA BARCA 3-2 ALLIANZ ARENA, LAKINI HAIJASAIDIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top