KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amehitimisha zama zake za kutamba katika soka ya nyumbani, baada ya jana kusaini Mkataba wa miaka minne kujiunga na klabu ya Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Ngassa anafuata nyayo za Watanzania wengine wachache waliowahi kucheza Afrika Kusini kama Yussuf Macho ‘Musso’, Nteze John, Bakari Malima, James Tungaraza (marehemu), Iddi Pazi, na Suleiman Matola.
Lakini kati yao hao wote hakuna aliyepata mafanikio au kucheza kwa muda mrefu, wengine wakirudi baada ya muda mfupi tu na wengine wakihamia nchi nyingine.
Simulizi za kusikitisha zaidi ni wachezaji wawili, James Tungaraza na Malima waliohamia Vaal Proffessionals wote wakitokea Yanga SC mwaka 1996.
Tungaraza alicheza mzunguko mmoja akarejea nyumbani kwa mapumziko- na akiwa kwake Magomeni, Dar es Salaam akatuhumiwa kumpiga dada muuza chapati, aliyefungua kesi ambayo mwishowe mshambuliaji huyo akatupwa jela.
IIidaiwa Mahakama ya Mwanzo Magemeni; dada muuza chapati alikwenda kudai fedha zake kwa Mke wa marehemu James asubuhi sana wenyewe bado wamelala. Ilidaiwa dada huyo aligonga sana hadi James akaamka kwa hasira na kwenda kumpiga vibao.
Dada akafungua kesi, James akakamatwa- kama masihara mwisho wa siku akahukumiwa kifungo cha miezi 10 jela. Ndoto za James kurejea Afrika Kusini zikafia hapo na alipokuwa jela alipata maradhi ambayo hayakumpa fursa ya kuishi muda mrefu baada ya kutoka, akafariki dunia.
Malima alirejea nyumbani kwa mapumziko baada ya msimu, akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akadaiwa kukutwa na dawa za kulevya.
Bahati nzuri kwake Malima kesi iliunguruma akanusurika, akaachiwa huru, lakini akapoteza nafasi ya kurejea Afrika Kusini. Akarejea Yanga SC.
Pazi alikwenda Indonesia na wengine walirejea nyumbani baada ya muda mfupi tu.
Ngassa, mume wa Radhia na baba wa Farida (8) na Faria (6), awali alipata nafasi kadhaa za kwenda kucheza nje, ikiwemo Marekani na Ulaya, lakini klabu zake (Yanga na Azam) ziligoma kumuuza.
Yanga ilikataa kumuuza Ngassa Norway na Azam ilikataa kumuuza Marekani- baadaye yeye mwenyewe akakataa kwenda Sudan kucheza kwa dau zuri pia.
Waswahili wanasema kama ipo, ipo tu- hatimaye Ngassa aliyefikisha miaka 26, Aprili 12 mwaka huu, ametimiza ndoto zake za kucheza nje, tena katika nchi nzuri tu inayoweza kukuza kiwango chake, Afrika Kusini.
Nyota kadhaa waliotamba katika soka ya Afrika Kusini kama Bunene Ngaduane wa DRC, Jonathan Mensah wa Ghana, Kennedy Mweene wa Zambia na watoto wa nyumbani, John Tlale, Siphiwe Tshabalala na Thabo Matlaba wamepita Free State na sera kubwa ya klabu hiyo ni kuvumbua vipaji na kuuza.
Mabosi wa Free State wamemuweka wazi Ngassa akifanya vizuri na kupata ofa nzuri zaidi sehemu nyingine atauzwa bila mizengwe.
Hakika hii ni fursa nyingine nzuri kwake Ngassa katika mustakabali wa maisha yake- ambayo kama ataitumia vizuri atakuja kupumzika kucheza akiwa na maisha mazuri.
Wasiwasi mmoja tu, wachezaji wengi wa Tanzania wamekuwa hawawezi kuvumilia kucheza nje ya nyumbani- na hapa lazima niwapongeze Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wapo katika msimu wa nne TP Mazembe ya Lubumbashi, DRC.
Kukumbuka nyumbani ndiyo sababu kubwa ya wachezaji wengi wa Tanzania kushindwa kucheza nje.
Shomary Kapombe alipatiwa nafasi Ufaransa, AS Cannes na akwa analipwa kuliko alivyokuwa analipwa Simba SC, lakini akaamu kurejea nyumbani na kusaini Azam FC.
Edibily Lunyamila akiwa katikati ya harakati za kutafutiwa timu Ujerumani mwaka 1996, akarejea Yanga SC kwa mapenzi tu.
Hadi wanampa Mkataba mrefu Ngassa, Free State wamemtathmini kiasi cha kutosha mchezaji huyo na kujiridhisha ana muda mrefu zaidi wa kucheza soka.
Ngassa anatakiwa kuwa na uvumilivu, subira na melengo- iwapo anataka siku moja kutajwa kama mwanasoka wa kihistoria Tanzania.
Baada ya kucheza klabu zote kubwa za Tanzania- Yanga, Simba na Azam FC- Ngassa alibakiza kuporomoka tu na siku moja kujisalimisha timu ndogo tena kutafuta riziki ya kuendesha familia.
Wazi hii ni bahati kwake- ambayo anapaswa kuitumia vizuri kupiga hatua zaidi mbele kisoka.
Hapaswi kubweteka na kuanza kufanyia anasa mshahara mzuri atakaokuwa anapata kuanzia Juni, matokeo yake kushusha kiwango chake na mwishowe akavunjiwa Mkataba.
Kufanya mazoezi katika Uwanja mzuri, vifaa bora vya michezo, mazingira mazuri na kucheza Ligi bora Afrika kama PSL, tena katika timu isiyo na presha kama Free State, Ngassa anataka nini zaidi katika maisha yake ya soka kwa sasa. Kama ni bahati, Ngassa anayo sasa tumuone.

.png)
0 comments:
Post a Comment