• HABARI MPYA

    Sunday, May 10, 2015

    ALLIANCE YAANZA KWA USHINDI LIGI YA MABINGWA

    Na Alex Sanga, MWANZA
    TIMU ya soka ya Alliance FC ya Mwanza imeanza vyema michuano ya Mabingwa wa soka wa Mikoa(RCL) baada ya kuifunga mabao 3-0 timu ya Bariadi kutoka Mkoani Simiyu.
    Mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja wa JK Nyerere Mkoani wilayani Mbulu mkoani Manyara.
    Mabao ya Alliance yalifungwa na Martin Kiggi dakika ya 25, Athanas Mdamu dakika ya 45 na David Richard dakika ya 82.
    Kocha Mkuu wa Alliance FC, Kessy Mziray amewashukuru vijana wake kwa ushindi huo na pia ameipongeza Bariadi FC kwa mchezo mzuri.
    Alliance FC imeanza vizuri Ligi ya Mabingwa 

    Kocha wa Bariadi FC, Asangateli Joel amesema kuwa vijana wake walichoshwa na safari ila ameahidi kushinda Mechi zilizobakia zote.
    Mechi nyingine zilizochezwa leo ni Watumishi FC imetoka sare ya 2-2 na RAS Kagera, Small Prison imeshinda 1-0 dhidi ya Madini SC.
    Ligi hiyo itaendelea Jumanne kwa michezo ya Alliance vs Small Prison, Mtwivila vs Watumishi, Baruti vs RAS Kagera, Madini vs Bariadi FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALLIANCE YAANZA KWA USHINDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top