• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    SCHOLES: MAN UNITED HII BORA YA MWAKA JANA

    KIUNGO wa zamani wa klabu ya Manchester United, Paul Scholes (pichani kulia) amesema kuwa timu hiyo inaonekana kucheza katika kiwango cha chini kwa msimu huu kuliko msimu uliopita licha ya kuwa kocha Louis Van Gaal ametumia kiasi kikubwa katika kufanya usajili.
    Kiungo huyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo kimoja cha televisheni huko nchini Uingereza amesema kuwa kocha huyo mholanzi anaonekana kuridhika na kufurahishwa kwa timu yake kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi nchini humo.
    Scholes ambaye alitundika daruga mwaka 2013 baada kucheza kwa muda mrefu aliyasema hayo jana mara baada ya Manchester United kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United huku pia akionekana kutoridhishwa na aina ya ufundishaji ya kocha Louis Van Gaal.
    "Anaonekana anafuraha kushika nafasi ya nne lakini timu hii inahitaji kuwepo katika mbio za ubingwa kwa sababu ametumia paundi milioni 150 katika usajili " alisema Scholes.
    Aidha Scholes amesema kuwa haipaswi kumlaumu sana kocha huyo kwa msimu huu kwani ndiyo msimu wa kwanza lakini kwa msimu ujao inabidi awaridhishe mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wanyonge tangu Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SCHOLES: MAN UNITED HII BORA YA MWAKA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top