• HABARI MPYA

    Thursday, March 05, 2015

    HII NDIYO SABABU BAFETIMBI ALIZIMIA UWANJANI JANA

    HATIMAYE sababu iliyofanya mshambuliaji wa klabu ya Swansea, Bafetimbi Gomis azimie uwanjani jana katika mechi waliyocheza dhidi ya Tottenham Hotspurs katika uwanja wa White Hart Lane imefahamika baada ya mchezaji huyo kuamua kufunguka leo hii.
    Gomis ambaye amekuwa mshambuliaji tegemezi wa ndege hao wa baharini, tangu aondoke Wilfred Bony, amesema kuwa alikuwa na matatizo mengi yaliyomfanya awe na msongo wa mawazo na hivyo kupelekea hali hiyo kumtokea hapo jana.

    "Nilikuwa na msongo mkubwa wa mawazo kutokana na matatizo ya afya aliyonayo baba yangu na hivyo nilipaswa kurudi Ufaransa nikamuone lakini nilishindwa"alisema Gomis
    "Nilisikitika kwa kushindwa kuisadia timu yangu lakini nashukuru mambo yanaenda sawa na kwa sasa naendelea vizuri "aliongeza.
    Kocha wa klabu ya Swansea Garry Monk alisema kuwa Gomis alitaka kurudi uwanjani baada ya kutolewa nje na kusema anajisikia vizuri lakini kocha huyo alikataa kumrudisha uwanjani ili kulinda afya yake na nafasi yake ikachukuliwa na mreno Nelson Oliviera.
    Hali hiyo ya kuzimia imewahi kumtokea Gomis mara tatu wakati akiichezea klabu ya Lyon huko nchini Ufaransa na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2009 wakati akifanya mazoezi na timu ya taifa ya Ufaransa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HII NDIYO SABABU BAFETIMBI ALIZIMIA UWANJANI JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top