REAL Madrid imeitoa Schalke 04 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kufungwa mabao 4-3 nyumbani, Uwanja wa Bernabeu.
Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4, baada ya awali kushinda ugenini, Ujerumani mabao 2-0.
Mwanasoka Bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana alimpiku Lionel Messi na Raul katika chati ya wafungaji bora wa kihistoria michuano ya Ulaya baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za 25 na 45. Mreno huyo sasa anafikisha mabao 78 katika michuano ya Ulaya, akimpiku Raul aliyefunga mabao 76 sawa na Messi.
Aidha, Ronaldo sasa anamfikia Messi katika chati ya wafungaji wa mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wote 75 kila mmoja, wakifuatiwa na Raul mabao 71, Ruud van Nistelrooy 56 na Thierry Henry 50.
Bao lingine la Real jana limefungwa na Karim Benzema dakika ya 52, mabingwa hao watetezi wakitinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
Mabao ya Schalke yalifungwa na Christian Fuchs dakika ya 20, Klaas-Jan Huntelaar mawili dakika za 40 na 84 na Leroy Sane dakika ya 57.
Katika mchezo mwingine wa jana, FC Porto imeifnga Basel mabao 4-0, hivyo kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya sare ya 1-1 awaloi ugenini.
Kikosi cha Real Madrid; Casillas, Arbeloa/Nacho dk83, Varane, Pepe, Fabio Coentrao/Marcelo dk58, Khedira/Modric dk58, Kroos, Isco, Ronaldo, Benzema na Bale.
Schalke: Wellenreuther, Howedes, Nastasic, Matip, Fuchs, Meyer, Neustadter, Hoger/Goretzka dk57, Barnetta/Uchida dk81, Choupo-Moting/Sane dk29 na Huntelaar.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo sasa ndiye mchezaji aliyefinga mabao mengi zaidi michuano ya Ulaya
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2988731/Cristiano-Ronaldo-overtakes-Lionel-Messi-Raul-highest-goalscorer-European-competitions-brace-against-Schalke.html#ixzz3U2vHt9Vg


.png)
0 comments:
Post a Comment