IEMMANUEL Okwi alifunga bao rahisi, akisaidiwa na makosa ya kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ kutoka bila ‘mahesabu’ langoni.
Lakini pia, kitendo cha wachezaji wa Yanga SC kucheza kwa mazoea, kwa kujifanya wameingia kwenye fikra za Okwi.
Namaanisha nini? Wachezaji wa Yanga SC hawakumbughudhi Okwi wakidhani angetoa krosi, au pasi- hivyo walijiandaa kuucheza mpira utakaoondoka kwenye himaya ya Mganda huyo.
Naye kama alisoma hisia za wachezaji wa Yanga na kwa kuona kosa la Barthez, akaamua kujaribu kufanya kitu ambacho mara kadhaa tumeshuhudia akikifanya kwa mafanikio.
Mabao ya aina ile Okwi amefunga sana na haikuwa mara ya kwanza Jumapili ya Machi 8, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga SC ikalala 1-0 katika mchezo wa marudiano, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Lakini kufungwa ni jambo moja, pili ni kwamba, Yanga SC walizidiwa uwanjani na Simba SC muda wote wa mchezo.
Mapema tu baada ya kupata orodha ya vikosi vya timu hizo vilivyoanza, nilithubutu kuwaambia watu niliokutana nao, kabla ya mchezo, kwamba Yanga inaweza kufungwa.
Ni kwa sababu ya upangwaji wa timu ya Simba SC, inayofundishwa na kocha Mserbia Goran Kopunovic ulikuwa makini mno.
Kopunovic alianzisha viungo watatu, wawili wakabaji. Abdi Banda na Jonas Mkude walikuwa viungo wa ulinzi wote, ambao timu inapokuwa na mpira wanasaidia mashambulizi, wakati Said Ndemla alicheza juu yao.
Yanga SC ilikuwa ina viungo wawili tu katikati, Said Juma ‘Kizota’ na Haruna Niyonzima na kwa sababu hiyo, haikuwa ajabu Smba SC ikatawala mchezo tangu mwanzo.
Nilitarajia kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm angeimarisha safu yake ya kiungo kwa kumuongeza Hassan Dilunga aliyekuwa benchi. Hapana. Hakufanya hivyo hata pale alipoamua kumtoa Danny Mrwanda dakika ya 30 baada ya kupoteza nafasi nzuri, akaongeza mshambuliaji Hussein Javu.
Baada ya dakika 45 kumalizika bila mabao, nikatarajia kabisa kipindi cha pili, Pluijm angeliona hilo- lakini wapi. Alirudi na timu ile ile.
Simba SC ikaendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 52, mfungaji Okwi.
Bado nidhamu ya uchezaji ya wachezaji wa Simba SC ilikuwa nzuri kuliko ya Yanga. Tulishuhudia akina Okwi, Ramadhani Singano ‘Messi’ wanashuka kuja kusaidia ulinzi.
Simba SC pamoja na mbinu nzuri za makocha, lakini wachezaji walikuwa wanajituma pia.
Mpira ni mchezo wa makosa, leo huwezi kumtupia lawama Barthez kwa kosa alilolifanya hadi akaruhusu bao, kwa sabahu hiyo ndiyo soka.
Kama ni lawama haswa, wanastahili kuzibeba makocha wa Yanga SC kwa kushindwa kung’amua mfumo wa wapinzani wao na kufanya marekebisho.
Yanga SC chini ya Pluijm, imekuwa ni timu inayopenda kushambulia na hujaza washambuliaji wengi uwanjani, lakini anasahau kwamba kunatakiwa kuwe na muuganiko na uwiano mzuri katika timu kutoka safu moja hadi nyingine.
Kama unatumia washambuliaji wanne, na viungo wawili, ukikutana na timu yenye viungo zaidi ya wawili, wazi washambuliaji wako watakuwa wanazurula tu uwanjani.
Tazama Kopunovic, baada ya kuwa anaongoza 1-0 na Yanga ikapoteza mchezaji mmoja, Haruna Niyonzima kwa kadi nyekundu, akapunguza kiungo mmoja, Abdi Banda na kuingiza mshambuliaji Simon Sserunkuma dakika za mwishoni.
Kopunovic aliacha benchi washambuliaji wake wawili mahiri, Dan Sserunkuma na Elias Maguri, hakuwa na tamaa ya kutumia washambuliaji wengi, bali viungo zaidi.
Yanga wenyewe ndiyo walioufanya mchezo wao uwe mgumu siku hiyo, kwa kujaza washambuliaji, viungo wachache.
Na hata kwa uongozi wa Yanga SC, nao unaweza kubeba lawama kwa matokeo ya jana- kwa kushindwa kutumia fursa ya kanuni mpya ya Ligi Kuu kuwaombea beki Juma Abdul na kiungo Salum Telela waliokuwa wana adhabu ya kadi za njano wacheze mechi hiyo muhimu, ili waje kupumzika mechi zijazo.
Kwa sasa, Telela ni mchezaji anayeifanya Yanga SC icheze, kutokana na umahiri wake katika safu ya kiungo. Alikosekana Jumapili.
Lakini hata Juma Abdul, yupo katika kiwango kizuri kwa sasa kucheza beki ya kulia, kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo.
Mbuyu Twite huwa anakuwa mzuri sana anapocheza ama kiungo mkabaji, au beki wa kati. Lakini kwa pembeni, sana utafurahia anavyorusha mipira kama amepiga kwa miguu.
Juma Abdul anapanda na kushuka vizuri. Anapiga krosi zake vizuri mno. Lakini Yanga SC wakajiamini wanaweza kucheza bila wawili hao.
Mechi ya Simba na Yanga, kama ambavyo inajulikana ya watani na wapinzai wa jadi, ni mechi ya kipekee ndiyo maana mapato Milioni 400 na zaidi.
Huwezi kuleta ujuaji wa kutaka kubadilisha uhalisia wa mechi hiyo kwa kusema eti unaichukulia ya kawaida huwezi kumuombea mchezaji mwenye kadi, acheze mechi hiyo aje kukosa nyingine wakati fursa ipo.
Yaani kwa ujumla, kipigo cha Yanga SC Jumapili ni cha kujitakia wenyewe na lawama za kwanza ni za makocha na viongozi. Alamsiki.

.png)
0 comments:
Post a Comment