• HABARI MPYA

    Friday, March 06, 2015

    MOHAMED SALAH AZIDI KUWASUTA CHELSEA, APIGA ZOTE MBILIFIORENTINA IKIILAZA JUVE 2-1

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah amewatumia ujumbe klabu yake, Chelsea baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 wa klabu yake ya mkopo, Fiorentina dhidi ya Juventus usiku wa jana.
    Kwa mabao hayo katika Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Italia, Salah sasa anafikisha jumla ya mabao sita katika mechi saba.
    Mabao hayo ya Salah aliyofunga dakika za 11 na 60, yanaifanya Juventus ipoteze mechi ya kwanza nyumbani baada ya mechi 48.
    Lazio imetoka sare na Napoli ya kufungana bao 1-1 katika Nusun nyingine ya Kombe la Mfalme na mechi za marudiano zitafanyika Aprili 7 na 8.
    Mohamed Salah opens the scoring with after a superb solo run from his own half against Juventus
    Mohamed Salah akimtoka mchezaji wa Juventus kabla ya kufunga bao la kwanza
    The Egypt international salutes the crowd after scoring against Serie A champions Juventus
    Mwanasoka huyo wa kimataifa akishangilia  oja ya mabao yake jana

    REKODI YA MABAO YA SALAH

    BASLE: Mechi 67, mabao 3.
    CHELSEA: Mechi 19, mabao mawili.
    FIORENTINA: Mechi saba, mabao sita
    EGYPT: Mechi 35, mabao 20. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOHAMED SALAH AZIDI KUWASUTA CHELSEA, APIGA ZOTE MBILIFIORENTINA IKIILAZA JUVE 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top