CHELSEA imetupwa nje ya michuano ya Ulaya kwa sare ya mabao ya ugenini, baada ya sare ya jumla ya 3-3 na PSG ya Ufaransa usiku wa kuamkia leo.
Hiyo inafuatia Chelsea kutoa sare ya 2-2 nyumbani baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 ugenini na timu hiyo ya Ufaransa.
Mabao ya David Luiz dakika ya 86 na Thiago Silva 114 yametosha kuitupa nje timu ya Jose Mourinho katika mchezo ambao Zlatanan Ibrahimovic alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya utata dakika ya 31 baada ya kumchezea rafu Oscar.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Gary Cahill dakika ya 81 na Eden Hazard dakika ya 96 kwa penalti baada ya Thiago Silva kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
KIkosi cha Cheksea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic/Zouma dk84, Ramires/Drogba dk91, Fabregas, Oscar/Willian dk46, Hazard na Costa.
PSG: Sirigu, Marquinhos, Thiago Silva, Luiz, Maxwell, Thiago Motta, Matuidi/Rabiot dk82, Verratti/Lavezzi dk82, Pastore/van der Wiel dk117, Cavani na Ibrahimovic.
David Luiz akienda juu zaidi ya Branislav Ivanovic kupiga kichwa kumtungua Thibaut Courtois jana
MBrazil huyo akishangilia bao lake jana
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2990463/Chelsea-2-2-PSG-Agg-3-3-Chelsea-away-goals-Zlatan-Ibrahimovic-sees-red-cynical-clash-Stamford-Bridge.html#ixzz3U8vi47M1


.png)
0 comments:
Post a Comment