• HABARI MPYA

    Monday, March 09, 2015

    BENZEMA BADO AIOTA BALLON D'OR

    MSHAMBULIAJI wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema amesema bado hajafuta ndoto zake za kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia licha ya kuwepo na ushindani mkali katika kinyang'anyiro hicho.
    Lionel Messi wa klabu ya Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid wanaonekana kuzitawala tuzo hizo kwa miaka ya hivi karibuni,Messi akichukua tuzo hizo mara nne na Ronaldo akibeba mara tatu katika kipindi hiki cha miaka 7.
    Hata hivyo mfaransa huyo amekataa kuzifuta ndoto zake hizo licha ya kukiri uwepo wa ushindani mkubwa hasa kutoka nyota hao wawili ambao wametawala ulimwengu wa soka kwa kipindi kirefu.

    "Hizi ndoto zangu siwezi kuzifuta.nitaongeza bidii na ninaamini siku moja nitanyanyua Ballon D'or. Hakuna mchezaji asiyependa kuchukua tuzo hiyo" alisema Benzema
    Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyejiunga na matajiri hao wa Hispania mwaka 2009 akitokea klabu ya Lyon na mpaka sasa ameshaifungia klabu hiyo zaidi ya magoli 80.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENZEMA BADO AIOTA BALLON D'OR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top