• HABARI MPYA

    Thursday, February 26, 2015

    TFF YAZITILIA UBANI AZAM, YANGA, KMKM NA POLISI MICHUANO YA AFRIKA

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitakia kila la kheri na ushindi timu za Azam na Yanga SC katika michezo yao ya marudiano itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii .
    Azam FC itakuwa ugenini siku ya jumamosi mjini Khartoum, Sudan kucheza mchezo wa marudiano na wenyeji timu ya El Merreikh ambapo katika mchezo wa awali uliofanyika Chamazi jijini Dar es salaam Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

    Jijini Gaborone nchini Botswana katika kombe la Shirikisho, timu ya Young Africans watacheza na wenyeji timu ya jeshi ya BDF XI siku ya ijumaa katika mchezo wa marudiano pia, ambapo katika mechi ya awali Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
    Mjini Zanzibar KMKM wataikaribisha timu ya AL Hilal ya Sudan siku ya jumamosi katika Uwanja wa Aman, huku kikosi hicho Maalum cha Kuzuia Magendo kikihitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kuweza kusonga mbele, kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza Khartoum kwa mabao 2-0.
    Timu ya Polisi Zanzibar itakuwa mwenyeji wa timu ya FC Mounana kutoka nchini Gabon siku ya jumapili katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika,ikihitaji ushindi wa mabao 5-0 ili kufuzu hatua inayofuata baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 4-0.
    Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, famili ya mpira na watanzania wote wanawatakia kila la kheri na ushindi katika michezo hiyo ya marudiano ambapo timu hizo zitakua zikipeperusha bendera ya Taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZITILIA UBANI AZAM, YANGA, KMKM NA POLISI MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top