• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2015

  30 WAITWA TWIGA STARS KWA AJILI YA ZAMBIA

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji 30 kitakachoingia kambini siku ya Jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka huu.
  Kaijage ametangaza program yake ya  mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.

  Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume,  imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
  Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
  Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 30 WAITWA TWIGA STARS KWA AJILI YA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top