• HABARI MPYA

    Tuesday, February 24, 2015

    NASRY KUJIUNGA NA ASPIRE FOOTBALL DREAM SENEGAL

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KINDA Nasry Daudi Aziz aliyezaliwa Agosti 21, 2001 amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar nchini Senegal.
    Mradi wa Aspire nchini ulianza mchakato wa kusaka vijana mwezi Machi - Mei, 2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.
    Watoto wa Aspire Academy mjini Dakar, Senegal

    Kijana huyo ni miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 walikuwepo nchini Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.
    Kituo cha Aspire kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.
    Nasry Daud Aziz anatarajiwa kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakua kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka miatano.
    Kutoka nchini Tanzania Nasry anakua ni kijana wa tatu kujiunga na kituo hicho, wengine ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NASRY KUJIUNGA NA ASPIRE FOOTBALL DREAM SENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top