• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 23, 2015

  AZAM WAIFUATA EL MERREIKH KWA MBINU ZA KIJESHI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Azam FC, wanatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Sudan na kufanyia mazoezi katika uwanja wa jeshi nchini humo.
  Azam inaondoka kesho na shirika la ndege la Kenya Airways leo usiku ambapo itafikia nchini Kenya na baadae kuunganisha safari hadi Sudan ambapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya El Merreikh, mchezo utakaochezwa Febuari 27 mwaka huu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema kikosi chao kinatarajia kuondoka kesho kikiwa na wachezaji 23 ambao wamesajiliwa CAF pamoja na benchi la ufundi ambapo msafara wao utakuwa wa watu 50.

  Alisema suala la maadalizi ya hotel tayari yameshakamilika ambapo kutakuwa na hotel mbili kwa ajili ya kufikia wachezaji pamoja na viongozi wa timu.
  “Katika suala la mazingira hatuna wasiwasi nayo tayari mwakilishi wetu, aliyetangulia Sudan ametupa taarifa zote kuhusu suala la uwanja ambao tutafanya mazoezi jeshini siku zote na siku moja kabla ya mechi kutumia uwanja tutakaocheza mechi,” alisema.
  Kawemba alisema kikosi chao kitafanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya kuondoka ambapo itasafiri jioni kuelekea Sudan na tayari kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya El Merreikh.
  Hata hivyo, kocha mkuu wa Azam, Joseph Omog alisema haumizi kichwa juu ya  Yanga kuendelea kuchanja mbuga katika safari yao ya kuelekea kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
  Yanga ilishinda michezo miwili mfululizo mfululizo dhidi ya Tanzania Prison na Mbeya Cuty, huku kikosi chake kushindwa kupata pointi sita katika michezo miwili ambapo ililazimika kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shootingi na Tanzania Prison ambapo kila mechi waambulia pointi moja.
  Alisema wachezaji wake walikosa umakini katika mchezo wao dhidi ya Prison na kusababisha kupata ushindi katika mchezo waliocheza nyumbani hivyo anaimani anajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.
  “Kwa sasa ligi ngumu, ninachokiangalia zaidi ni jinsi gani ya kupata pointi muhimu katika michezo iliyobakia suala la Yanga kuendelea kubaki kileleni hakuna tatizo zaidi ya kuangalia ni jinsi gani kukiandaa kikosi changu kutetea taji letu la ubingwa,” alisema.
  Omog alisema kulingana na ugumu wa ligi atahakikisha mara baada ya kurejea nchini akitokea Sudan kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya El Merreikh, wanajipanga kwa ajili ya kupata pointi muhimu katika michezo iliyobakia ya Ligi Hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM WAIFUATA EL MERREIKH KWA MBINU ZA KIJESHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top