• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 19, 2015

  YANGA SC, AZAM FC KATIKA VITA YA USUKANI LIGI KUU LEO, ATAKAYEPIGWA ATAMSOMA NAMBA MWENZAKE

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja viwili tofauti nchini.
  Timu mbili zinazoongoza mbio za taji, mabingwa watetezi, Azam FC na washindi wa pili wa msimu uliopita, Yanga SC zote za Dar es Salaam, zitakuwa ugenini leo kusaka pointi.
  Azam FC inayofundishwa na makocha watatu wa kigeni, Mcameroon Joseph Marius Omog, Mganda George ‘Best’ Nsimbe na Mkenya Ibrahim Shikanda watakuwa wageni wa Ruvu Shooting kilomita kadhaa baada ya kulimaliza Jiji la Dar es Salaam, huko Mlandizi mkoani Pwani.
  Yanga SC watakuwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo
  Azam FC watakuwa Uwanja wa Mabatini mjini Morogoro leo

  Timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), inayofundishwa na Mkenya, Thom Olaba imekuwa ngumu kufungwa Uwanja wa nyumbani, Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.
  Hata hivyo, Azam FC ilivuna pointi tatu na mabao matatu katika mechi za mwishoni mwa msimu uliopita kwenye Uwanja huo na leo itajaribu kufanya hivyo tena.
  Kwa upande wa Yanga SC, inayofundishwa na Mholanzi Hans van der Pluijm akisaidiwa na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa wao watakuwa wageni wa Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Prisons inayofundishwa na mwalimu mkongwe nchini, David Mwamwaja pamoja na historia yake ya kutotaka kufungwa nyumbani hususan na vigogo, lakini kwa kuwa katika hatari ya kushuka, leo inatarajiwa kupambana zaidi.
  Azam FC ina pointi 25 za mechi 13, sawa kabisa Yanga SC, lakini mabingwa hao watetezi wana mabao mawili zaidi katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa (GD).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC, AZAM FC KATIKA VITA YA USUKANI LIGI KUU LEO, ATAKAYEPIGWA ATAMSOMA NAMBA MWENZAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top