• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  MTIBWA SUGAR WACHEZEA KICHAPO CHA MIGAMBO MKWAKWANI

  MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameendelea kufanya vibaya licha ya kuanza msimu kwa kishindo, baada ya leo kufungwa bao 1-0 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Matokeo hayo, yanaifanya Mgambo itimize pointi 20 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 11, wakati Mtibwa inabaki na pointi zake 19 za mechi 16. 
  Bao pekee la Mgambo JKT jioni ya leo limefungwa na Balimi Busungu dakika ya 27, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Salim Kapinga. 
  Mgambo JKT wameifunga 1-0 Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WACHEZEA KICHAPO CHA MIGAMBO MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top