• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 18, 2015

  STARS MABORESHO KUCHEZA NA KOMBAINI YA TANGA LEO

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha pili cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars Maboresho  leo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombani ya jiji la Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.
  Mchezo huo wa kujipima nguvu ni sehemu ya program ya kocha mkuu Mart Nooj ya kupata nafasi ya kuona maendeleo ya wachezaji wake ambao anawaandaa kuwa wachezaji wa timu ya Taifa ya baadae.
  Kikosi cha Stars Maboresho kitakuwa uwanjani leo Tanga

  Mara baada ya mechi ya leo jioni jijini Tanga, timu hiyo itarejea jijini Dar es salaam ili kutoa fursa kwa wachezaji kujiunga na vilabu vyao kwa ajili ya michezo inayowakabili mwishoni mwa wiki ikiwemo Ligi Kuu ya Vodacom na Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS MABORESHO KUCHEZA NA KOMBAINI YA TANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top