• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  MAN UNITED YACHARAZWA 2-1 NA SWANSEA

  MANCHESTER United wamechapwa mabao 2-1 na Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Liberty jioni ya leo. 
  Ander Herrera alianza kuwafungia wageni, United dakika ya 28 baada ya pasi ya Wayne Rooney, kufuatia kazi nzuri ya Angel di Maria.
  Hata hivyo, shangwe za bao la United hazikudumu, baada ya Ki Sung-Yueng kuisawazishia Swansea dakika mbili baadaye akimalizia krosi ya Jonjo Shelvey, kabla ya Bafetimbi Gomis kuifungia la ushindi timu hiyo dakika ya 73.
  Kikosi cha Swansea kilikuwa; Fabianski, Naughton, Fernandez, Williams, Taylor, Cork, Shelvey/Amat dk90, Ki 7, Sigurdsson/Montero dk74 na Gomis, Routledge.
  Manchester United: De Gea, McNair/Valencia dk46, Jones, Rojo, Shaw/Young dk59, Blind, Herrera, Fellaini, Di Maria/Mata dk79, Rooney na Van Persie.
  David de Gea, arguably United's best player this season, dives in vain to stop Ki's shot finding the back of the net
  Kipa wa Manchester United, David de Gea akichupa bila mafanikio kujaribu kuzuia shuti la Sung-Yueng wa Swansea linalotinga nyavuni

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2962915/Swansea-2-1-Manchester-United-Ki-Sung-Yueng-Bafetimbi-Gomis-seal-double-Louis-van-Gaal-s-form-side.html#ixzz3SOxysRRh 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YACHARAZWA 2-1 NA SWANSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top