• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 28, 2015

  COASTAL YAIPIGA 1-0 MGAMBO, MVUA YAVUNJA MECHI YA STAND UTD NA KAGERA KAMBARAGE

  BAO pekee la Mganda Yayo Kato Lutimba limeipa ushindi wa 1-0 Coastal Union dhidi ya Mgambo JKT jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Mganda huyo alifunga bao hilo dakika ya 88 akimalizia pasi ya Suleima Kibuta, baada ya kuingia akitokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Ayoub Yahya. 
  Ushindi huo katika mechi ya kwanza Coastal ikiwa chini ya kocha wa muda, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ unaifanya ifikishe pointi 22 mechi 17.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbeya City imelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, wakati mchezo kati ya Stand United na Kagera Sugar ulisitishwa dakika ya 80 kutokana na mvua kubwa.
  Hadi mchezo unasitishwa, Stand walikuwa wanaongoza 1-0 na sasa mechi hiyo itamaliziwa kwa dakika 10 kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COASTAL YAIPIGA 1-0 MGAMBO, MVUA YAVUNJA MECHI YA STAND UTD NA KAGERA KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top