• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  MAMBO YAPO ARSENAL, CRYSTAL PALACE AFA 2-1 CHUMBANI KWAKE

  RAHA ipo kwa Washika Bunduki wa London, Arsenal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Santi Cazorla alifungua biashara kwa kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya nane kwa penalti, kufuatia mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck kuangushwa kwenye boksi.
  Olivier Giroud akawafungia The Guuners bao la pili dakika ya 45, wakati Glenn Murray aliifungia bao la kufutia unyonge Palace dakika ya 90. 
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Sanchez/Gabriel dk89, Ozil/Rosicky dk76, Welbeck/Gibbs dk76 na Giroud. 
  Crystal Palace: Speroni, Ward, Dann, Delaney, Souare, Ledley/Ameobi dk79, Zaha, Puncheon, Mutch, Gayle/Murray dk79 na Campbell/Bolasie dk57. 
  The Spanish midfielder celebrates after sending Julian Speroni the wrong way to put the Gunners a goal up at Selhurst Park
  Santi Carzolla akishangilia baada ya kuifungia The Gunners bao la kwanza leo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2962985/Crystal-Palace-1-2-Arsenal-Santi-Cazorla-Olivier-Giroud-strike-unconvincing-Gunners-Champions-League-spots.html#ixzz3SP0sokyt 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMBO YAPO ARSENAL, CRYSTAL PALACE AFA 2-1 CHUMBANI KWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top