• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  SIMBA SC KUMKOSA IVO MAPUNDA, MAMBO YOTE ‘DOGO’ PETER MANYIKA KAMBARAGE

  Na Princess Asia, SHINYANGA
  SIMBA SC itaendelea kumkosa kipa wake namba, Ivo Philip Mapunda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Voacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Stand United kesho Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya jicho.
  Baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Polisi Morogoro, Ivo alikwenda kutibiwa na kutakiwa kupumzika kwa wiki moja.
  Maana yake, katika wakati huu ambao kipa wa pili, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ naye ndiyo anafanya mazoezi ya kujiweka fiti baada ya kupona ugoko, Simba SC itabaki na kipa mmoja tu, Peter Manyika.
  Hakuna shaka kuhusu ‘bwana mdogo’ Manyika kulinda lango la Simba SC vizuri, lakini tatizo ni iwapo tu naye atapatwa na dhoruba kama ‘wakubwa’ zake.
  Simba SC kuna wakati ilimpandisha kikosi cha kwanza kipa wa kikosi cha vijana, ‘Simba B’ baada ya makipa wake wawili Casillas na Mapunda kuwa majeruhi, lakini shaka ni juu ya uwezo wake.
  Simba SC itamkosa Ivo Mapunda katika mchezo na Stand United mjini Shinyanga kesho

  Ivo amejikuta katika msimu mbaya, baada ya mapema tu mwanzoni mwa msimu kuumia kidole akiwa mazoezini katika kambi yao ya Zanzibar Septemba mwaka jana.
  Baada ya kupona kuanza taratibu Januari mwaka huu, ivo akaumia tena Jumapili Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kufuatia kubabuliwa jichoni na shuti la mshambuliaji wa Yanga SC, Saidi Bahanuzi anayecheza kwa mkopo Polisi. 
  Na kipa namba mbili wa timu hiyo, Casillas aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mtibwa Sugar aliumia ugoko Oktoba mwaka jana katika kambi ya Afrika Kusini.    
  Simba SC yenye pointi 20 za mechi 24, inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kuzisogelea Yanga SC na Azam FC kileleni mwa Ligi Kuu.
  Yanga SC inaongoza mbio za ubingwa wa Ligi Kuu kwa pointi zake 28 baada ya kucheza mechi 14, sawa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 26. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUMKOSA IVO MAPUNDA, MAMBO YOTE ‘DOGO’ PETER MANYIKA KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top