• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2015

  MEZ B WA EAST ZOO AFARIKI DUNIA

  MWANAMUZIKI Moses Bushagama maarufu kama Mez B amefariki dunia. Mez B alikuwa mmoja wa wanamziki wanaounda kundi la Chamber squard,amefariki leo mjini Dodoma kwa ugonjwa wa homa ya mapafu(TB). Mama yake amethibitisha kifo chake.
  Mez B atakumbukwa kwa vibao vyake vikali kama Kikuku, kama vipi, nimekubali na nyimbo ya Ghetto langu aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangea.
  Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea a.k.a Ngair huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen.
  Mez B enzi za uhai wake. Pumzika kwa amani Moses Bushagama

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MEZ B WA EAST ZOO AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top