• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 25, 2015

  MESSI AKOSA PENALTI, SUAREZ APIGA ZOTE MBILI BARCA IKIIKALISHA MAN CITY ETIHAD

  MANCHESTER City imesogea karibu na mlango wa kutokea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia kipigo cha mabao 2-1 nyumbani usiku huu Uwanja wa Etihad kutoka kwa Barcelona katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora.
  Mbaya wa City usiku huu alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez aliyeifungia Barcelona mabao yote hayo.
  Suarez, mfungaji bora wa zamani England alfunga bao la kwanza dakika ya 16 akiwa ndani ya boksi, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 30 akimalizia kazi nzuri ya Lionel Messi.
  Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la kufutia machozi zikiwa zimbeki dakika 21. City ilimpoteza Gael Clichy aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano na Messi akakosa penalti dakika ya mwisho.
  Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri/Fernandinho dk61, Milner, Fernando, Silva/Sagna dk78, Dzeko/Bony dk68 na Aguero. 
  Barcelona: Ter Stegen, Alves/Adriano dk75, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Rakitic/Mathieu dk71, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar/Pedro dk80.
  Suarez celebrates the crucial first away goal after finishing emphatically past Joe Hart, as Kompany looks despondent on his knees
  Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga akimtungua kipa Joe Hart, huku Nahodha wa Man City, Vincent Kompany akiwa amepiga magoti

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2967466/Manchester-City-1-2-Barcelona-Luis-Suarez-bites-double-former-Liverpool-striker-settles-old-scores-return-England.html#ixzz3Si7C2m8k 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AKOSA PENALTI, SUAREZ APIGA ZOTE MBILI BARCA IKIIKALISHA MAN CITY ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top