• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  MAN CITY WAFUFUA MAKALI, WAIFUMUA NEWCASTLE UNITED 5-0

  MABINGWA watetezi, Manchester City wamerudi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Newcastle United Uwanja wa Etihad usiku huu.
  City sasa inafikisha pointi 55 baada ya mechi 26, sawa na vinara, Chelsea wenye pointi 60 kileleni- na wanaendelea kuwa nafasi ya pili, mbele ya Manchester United wenye pointi 47 na Arsenal pointi 48.
  Vurnon Anita alifanya makosa yaliyoizawadia City penalti iliyowapa bao la kwanza sekunde ya 28, mfungaji Sergio Aguero, kabla ya Samir Nasri kufunga la pili dakika ya 12.
  Edin Dzeko akafunga la tatu dakika ya 21 kabla ya David Silva kufunga la nne dakika ya 51 na la tano dakika ya 53.
  Mshambuliaji wa Ivory Coast, Wilfried Bony aliichezea kwa mara ya kwanza Man City leo baada ya kusajiliwa dirisha dogo kutoka Swansea City, akiingia kuchukua nafasi ya Aguero kipindi cha pili.
  Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov; Nasri/Lampard dk70, Fernandinho, Toure, Silva/Navas dk59, Dzeko na Aguero/Bony dk60.
  Newcastle United; Krul, Janmaat/Taylor dk71, Williamson, Coloccini, Haidara, Sissoko, Anita/Abeid dk46, Colback, Gouffran/Obertan dk86, Cisse na Perez.
  David Silva offers a wave to the crowd after scoring City's fourth before adding a fifth moments later with a brilliant driven effort
  David Silva akiwapungia mkono mashabiki baada ya kufunga

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2963093/Manchester-City-5-0-Newcastle-United-David-Silva-brace-goals-Sergio-Aguero-Samir-Nasri-Edin-Dzeko-close-gap-Chelsea-five-points.html#ixzz3SPd9bNTa 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY WAFUFUA MAKALI, WAIFUMUA NEWCASTLE UNITED 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top