• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  KAGERA SUGAR WAISHUSHA AZAM FC LIGI KUU, SASA WAIPUMULIA YANGA SC KILELENI

  KAGERA Sugar wamepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Polisi Moro Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Kagera wanafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 17, wakiwashushia nafasi ya tatu mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 26 za mechi 14. Yanga SC yenye pointi 28 za mechi 14, inaongoza Ligi Kuu.
  Bao pekee Kagera leo limefungwa na mshambuliaji wa ‘Taifa Stars Maboresho’, Rashid Mandawa.
  Katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, wenyeji Ndanda wameshinda 1-0 dhidi ya Coastal Union, bao pekee la Nassor Kapama.
  Kagera Sugar wamepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAISHUSHA AZAM FC LIGI KUU, SASA WAIPUMULIA YANGA SC KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top