BONDIA Manny Pacquiao amempa ofa ya dola za Kimarekani Milioni 5 mpinzani wake, Floyd Mayweather Jnr iwapo atafeli vipimo vya kama anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizpigwa mchezoni.
Mfilipino huyo ametoa ofa hiyo kuelekea pambano lao kali linalosubiriwa kwa hamu lenye thamani ya Pauni Milioni 200 Mei mwaka huu.
Pacquiao, ambae pia amethibitisha pambano hilo linakuja, amekubali sharti la Mayweather kufanyiwa vipimo katika mtindo wa michezo ya Olimpiki.
Mmarekani, Mayweather anatarajiwa kutangaza kukubali kuzipiga na nyota wa Filipino mjini Las Vegas, Marekani Mei 2, 2015.
Mayweather na Pacquiao wakizungumza baada ya kukutana uso kwa uso kwenye Uwanja wa mpira wa kikapu hivi karibuni
0 comments:
Post a Comment