• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 28, 2015

  SUAREZ AENDELEZA MOTO WA MABAO BARCA IKIPIGA MTU 3-1 LA LIGA

  TIMU ya Barcelona imeifunga Granada mabao 3-1 katika La Liga jioni ya leo na kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara Real Madrid hadi kubaki moja. 
  Ivan Rakitic aliwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 26, kabla ya Luis Suarez kuongeza la pili dakika ya kwanza kipindi cha pili.
  Fran Rica akaifungia bao la kufutia machozi Granada dakika tano baadaye kwa penalti baada ya Marc Bartra kumuangusha Lass Bangoura- kabla ya Lionel Messi kuifungia timu ya Luis Enrique bao la tatu zikiwa zimebaki dakika 20.
  Granada: Oier; Nyom, Babin, Cala, Foulquier; Iturra, Rico, Marquez/Rochina dk67, Bangoura/Candeias dk79, Ibanez na Cordoba/Isaac 78.
  Barcelona: Bravo; Alves, Bartra, Mathieu/Busquets dk75, Alba, Mascherano, Xavi/Rafinha dk65, Rakitic, Messi, Neymar na Suarez/Pedro dk79.
  Suarez wheels away in celebration after doubling the lead for Luis Enrique's side minutes after half time on Saturday
  Suarez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu ya Luis Enrique leo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2973532/Granada-1-3-Barcelona-Luis-Suarez-Lionel-Messi-target-Catalans-ramp-pressure-league-leaders-Real-Madrid.html#ixzz3T3vKR600 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUAREZ AENDELEZA MOTO WA MABAO BARCA IKIPIGA MTU 3-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top