• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2015

  BINGWA TRACE MUSIC APATIKANA, ALAMBA MILIONI 50 ZA AIRTEL

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel, leo imemtangaza rasmi mshindi wa shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa
  miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza kuimba na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa lengo la kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.
  Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na kupigiwa kura na Watanzania.

  Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga mfano wa hundi ya Sh. Milioni 50, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya
  Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi, anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

  "Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae
  majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5)" alifafanua Muga.
  Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050),  Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya  (55100366).
  Mshindi ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182) ambaye amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na
  wananchi.
  Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika Nairobi Kenya yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za kimataifa nchini Uingereza, na kupewa mafunzo toka kwa msanii nguli wa Afrika, Akon.
  Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya vijana 13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Kongo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo (DRC) na Gabon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BINGWA TRACE MUSIC APATIKANA, ALAMBA MILIONI 50 ZA AIRTEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top