• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 22, 2015

  AZAM FC WAANZA KUISHINDWA KASI YA YANGA, WABANWA 0-0 NA PRISONS CHAMAZI

  AZAM FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons ya Mbeya usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanamaanisha, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 27, baada ya kucheza mechi 15, wakizidiwa kwa pointi nne na vinara, Yanga SC wenye pointi 31 za mechi 15 pia.
  Sare hiyo ya pili mfululizo kwa timu hiyo inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog inamaanisha Azam FC inaelekea kuuweka rehani ubingwa.

  Yanga SC, imeendeleza wimbi la ushindi mjini Mbeya, baada ya leo kuwafunga Mbeya City mabao 3-1 Uwanja wa Sokoine- kufuatia katikati ya wiki kuwafunga Prisons 3-0.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe, wakati bao pekee la Mbeya City limefungwa na Peter Mapunda.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Simba SC imelala 1-0 mbele ya Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, bao pekee la Abaslim Chidiaebele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAANZA KUISHINDWA KASI YA YANGA, WABANWA 0-0 NA PRISONS CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top