// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAID BAHANUZI ALIYEONEKANA ‘GALASA’ YANGA AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAID BAHANUZI ALIYEONEKANA ‘GALASA’ YANGA AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 17, 2015

    SAID BAHANUZI ALIYEONEKANA ‘GALASA’ YANGA AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Said Rashid Bahanuzi (pichani juu) aliyetolewa kwa mkopo Polisi Morogoro na Yanga SC Desemba mwaka jana kwa sababu alionekana hana mchango katika hiyo, ameanza kuisuta timu hiyo ya Jangwani. 
    Hiyo inafuatia mfungaji huyo bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwaka 2012 akiwa na Yanga aliyoipa taji hilo kwa mabao yake, kuchaguliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzaia Bara mwezi huu. 
    Bahanuzi amekua na mchango mkubwa kwa timu yake mpya, tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini akitokea Jangwani.
    Naye kiungo wa Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Desemba 2014 baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu yake hiyo hivyo kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.
    Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
    Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAID BAHANUZI ALIYEONEKANA ‘GALASA’ YANGA AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top