• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  AZAM TV ‘KURUSHA LIVE’ FAINALI DARAJA LA KWANZA MWADUI NA AFRICAN SPORTS CHAMAZI

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  FAINALI ya kumsaka bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
  Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TTF), umepelekwa Chamazi.

  Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.
  Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.
  Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM TV ‘KURUSHA LIVE’ FAINALI DARAJA LA KWANZA MWADUI NA AFRICAN SPORTS CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top