• HABARI MPYA

    Thursday, February 19, 2015

    RAIS KIKWETE AMUIBUA TENA MWAKALEBELA 'WA TFF'

    RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya wapya 27 lakini katika idadi hiyo jina la Katibu Mkuu wa zamazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Wilfred Mwakalebela limo ndani yake.
    Mwakalebela amepata ulaji huo ambapo sasa anakwenda kuiongoza wilaya ya Wangingíombe iliyopo Njombe huku mwanahabari Shabani Kissu akipelekwa Kondoa.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Mwakalebela ambaye alikuwa katibu mkuu wa kwanza katika utawala wa Rais Leodegar Tenga amesema ameishukuru serikali kwa kuona mchango wake kwamba anaweza kuisaidia nchi yake.
    "Kwanza niishukuru serikali kupitia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa kunioan bado nina mchango wa kuisaidia nchi yangu lakini baada ya hilo nataka kufika katika kibarua changu hicho kujua changamoto zinaziwakabili wananchi wa huko,"alisema Mwakalebela.
    "Nikishafanya utambuzi huo sasa nitaanza mikakati ya kuanza utatuzi kwa haraka nikisaidiana na wananchi wa huko, kikubwa naomba ushirikiano kwa wakazi wenzangu wa Wang'ing'ombe.".
    Rais Kikwete akiwa na Mwakalebela kulia (Picha ya Maktaba)

    Kwa ujumla, Rais Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI mchana wa Jumatano, (Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
    Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
    Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wangingíombe.
    Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiangíombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
    Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
    Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
    Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS KIKWETE AMUIBUA TENA MWAKALEBELA 'WA TFF' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top