MWISHONI mwa wiki baadhi ya wanachama wa Simba SC kutoka kundi maarufu la Ukawa walipigwa na wanachama wenzao wa timu hiyo, wakituhumiwa kuisaliti timu hiyo katika mechi za ligi.
Inadaiwa wanachama wa Simba SC wa kundi la Ukawa wanataka timu ifanye vibaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na eti wanatumia uchawi, au ndumba kufanikisha hila zao hizo.
Mimi si muumini wa ushirikina na wakati wote, siku zote nachukulia kama uzushi tu na upotoshaji, pengine kutokana na imani yangu labda ya kidini, lakini ukweli wa mambo ndiyo huo Simba SC.
Jumapili, baadhi ya wanachama wa Simba SC wa kundi la Ukawa walipigwa na wenzao mjini Morogoro eti baada ya kukamatwa na ndumba ambazo walipeleka ili timu ifanye vibaya mbele ya wenyeji Polisi.
Na haikuwa mara ya kwanza wapenzi hao wa Simba wa Ukawa kufanyiwa fujo na wenzao, bali imewahi kutokea mara kadhaa pia chini ya uongozi wa sasa, wa Rais Evans Elieza Aveva.
Na hawa Ukawa ambao sasa wanadaiwa kuwa maadui wa uongozi uliopo madarakani hivi sasa, ni wale ambao walikuwa maswahiba wa Rais aliyemaliza muda wake, Alhaj Ismail Aden Rage.
Na tulishuhudia wakati wa Rage, hakuwa na amani ya utawala kutokana na misukosuko iliyotokana na jitihada za kumpinga, hadi kufikia kumpindua.
Na wakati huo, Rage alikuwa analia na kundi la Friends Of Simba kwamba ndilo lilikuwa linamnyima raha madarakani kwa kuongoza uasi dhidi yake.
Na leo, kundi la Friends Of Simba ndilo limeshika hatamu klabuni kupitia memba wake wa muda mrefu, Aveva aliyeukwaa Urais wa klabu.
Rejea mchakato wa uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo mwaka jana, mgombea Michael Richard Wambura aliyeonekana kuungwa mkono na Rage, alienguliwa na baadaye akafutwa uanachama kwa tuhuma za kuipeleka klabu mahakamani, jambo ambalo ni kinyume cha muongozo FIFA.
Kweli, FIFA inakataza kabisa mambo ya mchezo wake kupelekwa kwenye mahakama za dola na hakuna shaka Wambura alikosea.
Wakati Jamal Malinzi anakuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwaka juzi, mara tu baada ya kutangazwa mshindi, jambo la kwanza alilofanya ni kuwasamehe wale wote waliokuwa wana adhabu mbalimbali, akisema “Tunaanza upya”.
Malinzi hakuwa na nia nyingine, zaidi ya kutaka kujenga umoja ndani ya soka ya Tanzania, ingawa naye baadaye ameingia kwenye mtego wa chuki na uadui na watu mbalimbali.
Kitu kimoja ambacho Aveva anafanya na matokeo yake kinamtengenezea mazingira magumu kiutawala, ni kuruhusu makundi ndani ya klabu.
Simba SC kuna makundi kuanzia kwenye Kamati ya Utendaji, matawi hadi vikundi vya ushangiliaji vinalalamika kubaguliwa.
Kauli mbiu ya SImba SC ni “Nguvu Moja”- lakini huwezi kuiona maana halisi ya kauli hiyo chini ya utawala wa Aveva, ikiwa ameruhusu matabaka kuanzia ndani ya Kamati ya Utendaji.
Naweza kuandika mambo ambayo yatamfurahisha sana Aveva, au kiongozi mwingine wa Simba SC, lakini yasiisaidie hata chembe klabu hiyo. Naweza.
Lakini kwa kuzingatia maslahi ya klabu, yanipasa kidogo kuweka kando urafiki na kujuana na kuandika kile ambacho naamini kinaweza kuwa na maslahi na klabu.
Ukweli ni kwamba, Simba SC inahitaji kuwa na umoja na baada ya hapo waanze upya kuwatafuta watu ambao si wema kwa klabu.
Kuanzia katika Kamati ya Utendaji, watu wote wajitakase, waweke kando chuki zao na kutanguliza maslahi ya Simba SC mbele.
Baada ya hapo, Kamati ya Utendaji yenyewe ibebe jukumu la kurejesha umoja baina ya wapenzi, wanachama na wana Simba wote kwa ujumla.
Kama Simba ni moja, kwa nini washikane uchawi wenyewe ka wenyewe. Kwa nini wagombane wenyewe. Kwa nini wasipendane. Yaani huwezi kuiona maana ya kaulimbiu ya Simba SC “Nguvu Moja” kwa sasa.

0 comments:
Post a Comment