• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 22, 2015

  AZAM FC NA YANGA SC KATIKA VITA YA ‘UBOSI’ LIGI KUU LEO, SIMBA SC NA STAND UNITED

  ‘FARASI’ wawili wanaokimbizana katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na Azam leo, wapo kwenye harakati tena.
  Yanga SC watacheza mechi yao ya mwisho mjini Mbeya, kwa kumenyana na wenyeji Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini humo baada ya katikati ya wiki kushinda 3-0 dhidi ya Prisons.
  Baada ya sare ya 0-0 katikati ya wiki Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya Ruvu Shiiting, mabingwa watetezi, Azam FC leo watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 


  Wiki mbili zilizopita, Yanga SC iliifunga Mtibwa 2-0 katika Ligi Kuu na siku tatu baadaye, Azam FC ikaifunga timu hiyo ya Manungu mabao 5-2.
  Watu wana hamu ya kuona mambo yatakuwaje kwa Prisons mbele ya Azam FC leo, wakitoka kukung’utwa 3-0 na Yanga SC.
  Yanga SC kwa sasa ndiyo wapo kileleni kwa pointi zao 28 za mechi 14, wakati Azam FC ina pointi 26 za mechi 14 pia.
  Uwanja wa Kambareg mjini Shinyanga, mabingwa wengine wa zamani wa Ligi Kuu watakuwa wageni wa Stand United.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC NA YANGA SC KATIKA VITA YA ‘UBOSI’ LIGI KUU LEO, SIMBA SC NA STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top