• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2015

  DILI LA MAN CITY KWA DIEGO SIMEONE LADUNDA, WENYE MALI WANG'ANG'ANIA MZIGO

  MPANGO wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City kumchukua kocha Diego Simeone unaelekea kukwama baada ya klabu yake, Atletico Madrid kuanza mazungumzo naye arefushe Mkataba wake hadi mwaka 2022.
  Dada wa kocha huyo Muargentina, Natalia Simeone, ambaye anashughulikia masuala yake ya kimikataba, amekuwa katika Jiji la Hispania kwa siku 10 zilizopita kujadili vipengele vya Mkataba mpya.
  Mabingwa hao watetezi La Liga, ambao hivi karibuni wameuza asilimia 20 ya hisa zao kwa kampuni ya Dalian Wanda Group, wana nia thabiti ya kumbakiza kwa muda mrefu kocha huyo, baada ya miaka saba ya kufanya naye kazi kwa mafanikio.
  The 44-year-old Argentinian is reportedly in talks over extending his contract at Atletico until 2022

  MANCINI AMEKALIA KUTI KAVU MAN CITY 

  Mustakabali wa kocha Manuel Pellegrini ndani ya Etihad unaweza kuamuliwa na mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya juzi kufungwa mabao 2-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza mjini Manchester.
  Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa ni kumpa mamlaka kamili Simeone mwenye umri wa miaka 44 juu ya kusajili wachezaji.
  Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Argentina amekuwa lulu Uwanja wa Vicente Calderon, baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ya Hispania na kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako walifungwa na wapinzani wao, Real Madrid msimu uliopita.
  Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kutaka kumchukua Simeone ili kuimarisha kikosi chake na hatimaye kukata kiu ya kushinda mataji zaidi, yakiwemo ya Ulaya.
  City imetolewa kwenye mashindano yote ya vikombe England, wakati kwenye Ligi Kuu kwa sasa wanazidiwa pointi sana na vinara, Chelsea.
  Manuel Pellegrini's future at the Etihad is uncertain should he end the season without winning silverware
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DILI LA MAN CITY KWA DIEGO SIMEONE LADUNDA, WENYE MALI WANG'ANG'ANIA MZIGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top