• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 28, 2015

  MAREFA WA ZAMBIA WAITUPA NJE AZAM FC LIGI YA MABINGWA

  AAZAM FC imeaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufungwa mabao 3-0 na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali uliofanyika Uwanja wa Marreikh mjini Khartoum.
  Marefa wa mchezo huo kutoka Zambia Wellington Kaoma aliyesaidiwa na Romeo Kasengele na Amos Nanga walionekana wazi kuiuma Azam FC katika mchezo huo.
  Pamoja na kupewa penalti ambayo iliokolewa na kipa Aishi Manula, Merreikh ilimaliza dakika 45 za kwanza inaongoza 1-0.
  Refa wa Zambia Wellington Kaoma leo ameimaliza Azam FC Sudan kwa kuibeba Merreikh

  Kipindi cha pili marefa wa Zambia waliongeza mbeleko kwa Merreikh na ikafanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyofungwa na Ahmed Abdallah dakika ya 85 na Alan Wanga dakika ya 90.
  Azam FC inatolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kwa kujua mbinu walizopanga na marefa hao, Merreikh walizuia mchezo huyo usionyeshwe na Televisheni yoyote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA ZAMBIA WAITUPA NJE AZAM FC LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top