• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 25, 2015

  CARLOS TEVEZ ATIA MOJA KWENYE KAMBA JUVE IKIICHAPA DORTMUND LIGI YA MABINGWA ULAYA

  MABINGWA wa zamani Ulaya, Juventus wameizaba mabao 2-1 Borussia Dortmund usiku huu katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Italia.
  Juve au Kibibi Kizee cha Turin, ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Carlos Tevez dakika ya 13 aliyetumia makosa ya kipa Roman Weidenfeller.
  Lakini Borussia Dortmund ikafanikiwa kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Marco Reus aliyetumia udhafu wa beki, Giorgio Chiellini kabla ya Alvaro Morata kuifungia bao la ushindi Juve dakika ya 43.
  Dortmund kwa kupata bao le ugenini, imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kuelekea mchezo wa marudiano Machi 18 Uwanja wa Westfalenstadion.
  Kikosi cha Juventus kilikuwa: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo/Pereyra dk37, Pogba, Vidal/Padoin dk86, Tevez/Coman dk89 na Morata.
  Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek/Ginter dk32, Papastathopoulos/Kirch dk46, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Sahin, Aubameyang, Mkhitaryan, Reus na Immobile/Blaszczykowski dk75.
  Tevez celebrated his fourth goal in the Champions League this year with a dummy in his mouth as Juventus took an early lead
  Carlos Tevez akishangili bao lake ka nne katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2967367/Juventus-2-1-Borussia-Dortmund-Carlos-Tevez-Alvaro-Morata-seal-Champions-League-16-leg-win-Italian-champions.html#ixzz3SiAFFfit 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CARLOS TEVEZ ATIA MOJA KWENYE KAMBA JUVE IKIICHAPA DORTMUND LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top