• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2015

  STARS YAPANGWA NA ZIMBABWE KUWANIA ROBO FAINALI KOMBE LA CASTLE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imepangwa pamoja na Namibia, Lesotho na Zimbabwe katika Kundi A la michuano ya Kombe la COSAFA.
  Katika droo iliyopangwa jioni ya leo mjini Johannesburg, Afrika ambako itafanyika michuano hiyo Mei mwaka huu, Kundi B lina timu za  Shelisheli, Madagascar, Mauritius na Swaziland.
  Kila timu itakayoongoza kundi, itaungana na wenyeji Afrika Kusini, Botswana, Ghana na Malawi, Msumbuji na Zambia kwa ajili ya hatua ya Robo Fainali.

  Mpinzani wa Tanzania katika hilo, anatarajiwa kuwa Zimbabwe, ambaye hata hivyo alitolewa na Taifa Stars katika mechi za kufuzu AFCON mwaka jana.
  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia zimeingia moja kwa moja katika Robo Fainali kwa sababu zipo juu viwango vya ubora wa soka vya FIFA.
  Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
  Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mayotte, Msumbuji, Namibia, Reunion, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe, lakini katika kuiongezea ladha ya ushindani, sasa hivi zinaalikwa na timu kutoka nje ya ukanda huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS YAPANGWA NA ZIMBABWE KUWANIA ROBO FAINALI KOMBE LA CASTLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top