• HABARI MPYA

    Thursday, February 26, 2015

    JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA MACHI 22

    HATIMAYE makundi mawili yanayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi katika taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic yatafanya onyesho la pamoja mwezi ujao.
    Onyesho hilo litafanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 22 mwezi Machi.
    Hii inakuwa ni mara ya pili kwa makundi hayo mawili kufanya onyesho la pamoja (bila kushirikishwa makundi mengine).
    Onyesho la kwanza lililopewa jina la Usiku wa Baba na Mwana lilifanyika miaka minne iliyopita ndani ya ukumbi huo huo na inaaminika kuwa hadi leo bado rekodi yake ya mahudhurio pale Travertine haijavunjwa.
    Mzee Yussuf na Isha Mashauzi ambao ni wamiliki wa makundi hayo, wameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni “Usiku wa Baba na Mwana …Season 2”.
    Viongozi hao wamesema onyesho hilo ni la kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashabiki wao na kamwe halina hata chembe ya wala mpambano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA MACHI 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top