• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND

  CHELSEA imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley Uwanja wa Stamford Bridge jioni ya leo. 
  Branislav Ivanovic alifunga bao lake la pili wiki kwa kikosi cha Jose Mourinho dakika ya 14 kuipatia Chelsea bao la kuongoza, kabla ya mchezaji mwenzake, Nemanja Matic kutolewa kwa kadi nyekundu.
  Matic alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumrudishia kipigo Ashley Barnes aliyemchezea rafu dakika ya 70.
  Beki wa pembeni wa Burnley, Ben Mee aliisawazishia timu yake dakika ya 81.
  Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Zouma, Terry, Luis/Drogba dk85, Fabregas, Matic, Cuadrado/Willian dk63, Oscar/Ramires dk72, Hazard na Costa.
  Burnley; Heaton, Trippier, Shackell, Keane, Mee, Boyd, Jones, Arfield, Kightly/Vokes dk79, Barnes na Ings.
  Chelsea midfielder Cesc Fabregas catches Burnley's Kieran Trippier in the face with his arm during a challenge
  Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas akimkaba mchezaji wa Burnley, Kieran katika mchezo wa leo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2963036/Chelsea-1-1-Burnley-Ben-Mee-cancels-Branislav-Ivanovic-strike-Nemanja-Matic-sees-red-Blues-dealt-title-blow.html#ixzz3SP4Kqrzq 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAVUTWA MIGUU DARAJANI, 1-1 NA BURNLEY LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top