• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 27, 2015

  NGASSA AIPAISHA YANGA SC MICHUANO YA AFRIKA, YASONGA MBELE LICHA YA KUPIGWA 2-1

  Na Mwandishi Wetu, GABORONE
  BAO la Mrisho Khalfan Ngassa limeipeleka Yanga SC Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana kwa bao la ugenini.
  Yanga SC usiku huu imefungwa mabao 2-1 na BDF Uwanja wa Lobatse na BDF na kufanya isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam.
  Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 30 kwa kichwa, akimalizia pasi ya Amissi Tambwe ambaye alipokea krosi ya Simon Msuva.
  Mrisho Ngassa (kushoto) kwa mara nyingine leo ameonyesha umuhimu wake Yanga SC

  Mapema dakika ya 21, BDF walipata pigo baada ya beki wake, Othusitse Mpharitlhe kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kumfuatia kumchezea rafu winga wa Yanga SC, Simon Msuva. 
  Kipidi cha pili BDF waikianza vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Mosimanyana aliyemalizia kazi nzui ya Lerole.
  Dakika ya 72 mshambuliaji Danny Mrwanda alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu beki wa BDF.
  BDF walipata bao la pili dakika ya 85 kupitia kwa Kumbulani Madziba aliyewatoka mabeki wa Yanga kabla ya kumtungua Ally Mustafa ‘Barthez.’
  Yanga SC sasa watamenyana na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimababwe katika Raundi ya Kwanza. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Barthez, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Cannavaro, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa/Kpah Sherman dk87.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AIPAISHA YANGA SC MICHUANO YA AFRIKA, YASONGA MBELE LICHA YA KUPIGWA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top